Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 111 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَقَالُواْ لَن يَدۡخُلَ ٱلۡجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰۗ تِلۡكَ أَمَانِيُّهُمۡۗ قُلۡ هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ﴾
[البَقَرَة: 111]
﴿وقالوا لن يدخل الجنة إلا من كان هودا أو نصارى تلك أمانيهم﴾ [البَقَرَة: 111]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mayahudi na Wanaswara, kila mmoja katika wao anadai kuwa Pepo itaingiwa na pote lake peke yake, hataingia asiyekuwa katika pote hilo. Hayo ni mawazo yao maovu. Waambie, ewe Mtume, “Leteni dalili yenu juu ya ushahidi wa hilo mnalolidai iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu.” |