Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 126 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِـۧمُ رَبِّ ٱجۡعَلۡ هَٰذَا بَلَدًا ءَامِنٗا وَٱرۡزُقۡ أَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلثَّمَرَٰتِ مَنۡ ءَامَنَ مِنۡهُم بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُۥ قَلِيلٗا ثُمَّ أَضۡطَرُّهُۥٓ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلنَّارِۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ ﴾
[البَقَرَة: 126]
﴿وإذ قال إبراهيم رب اجعل هذا بلدا آمنا وارزق أهله من الثمرات﴾ [البَقَرَة: 126]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Kumbuka, ewe Nabii, wakati Aliposema Ibrāhīm akiwa katika maombi, “Ewe Mola wangu! ijaalie Makkah ni mji wenye amani usiokuwa na kitisho, uwaruzuku watu wake aina ya matunda na uwahusu kwa riziki hii wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” Mwenyezi Mungu Alisema, “Na mwenye kukufuru katika wao nitamruzuku ulimwenguni na kumstarehesha starehe chache, kasha nitamlazimisha kwa nguvu kwenda Motoni. Ubaya wa marejeo na makao ni mwisho huu.” |