Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 125 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿وَإِذۡ جَعَلۡنَا ٱلۡبَيۡتَ مَثَابَةٗ لِّلنَّاسِ وَأَمۡنٗا وَٱتَّخِذُواْ مِن مَّقَامِ إِبۡرَٰهِـۧمَ مُصَلّٗىۖ وَعَهِدۡنَآ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيۡتِيَ لِلطَّآئِفِينَ وَٱلۡعَٰكِفِينَ وَٱلرُّكَّعِ ٱلسُّجُودِ ﴾
[البَقَرَة: 125]
﴿وإذ جعلنا البيت مثابة للناس وأمنا واتخذوا من مقام إبراهيم مصلى وعهدنا﴾ [البَقَرَة: 125]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Kumbuka, ewe Nabii, wakati tulipoifanya Alkaba ni marejeo ya watu; wanakuja kuikusudia, kisha wanarudi makwao kwa watu wao, kisha wanairudia tena, ni makusanyiko yao katika Hija, Umra, kutufu na kuswali, na pia ni amani kwao: hakuna adui anayewashambulia wakiwa hapo na tukasema, “Pafanyeni hapo Maqām Ibrāhīm ni mahali pa kuswali. Maqām Ibrāhīn ni jiwe ambalo Ibrāhīm alisimama juu yake alipokuwa akijenga Alkaba. Na tulimletea Wahyi Ibrahīm na mtoto wake Ismāīl kwa kuwaambia, «Isafisheni Nyumba Yangu na kila najisi na uchafu kwa ajili ya wenye kuabudu kwa kutufu pambizoni mwa Alkaba au kuketi Itikafu (I’tikāf) Msikitini na kuswali hapo.” |