Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 163 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَإِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلرَّحۡمَٰنُ ٱلرَّحِيمُ ﴾
[البَقَرَة: 163]
﴿وإلهكم إله واحد لا إله إلا هو الرحمن الرحيم﴾ [البَقَرَة: 163]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mola wenu, enyi watu, ni Mola Mmoja Aliyepwekeka katika dhati Yake, majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake na uja wa viumbe Vyake Kwake. Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, Mwingi wa rehema, Mwenye kusifika kwa sifa ya rehema katika dhati Yake, vitendo Vyake kwa waja Wake wote, na Mwenye kuwarehemu waumini |