×

Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, 2:164 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:164) ayat 164 in Swahili

2:164 Surah Al-Baqarah ayat 164 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 164 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿إِنَّ فِي خَلۡقِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱخۡتِلَٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ وَٱلۡفُلۡكِ ٱلَّتِي تَجۡرِي فِي ٱلۡبَحۡرِ بِمَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ وَمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن مَّآءٖ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَآبَّةٖ وَتَصۡرِيفِ ٱلرِّيَٰحِ وَٱلسَّحَابِ ٱلۡمُسَخَّرِ بَيۡنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ ﴾
[البَقَرَة: 164]

Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن في خلق السموات والأرض واختلاف الليل والنهار والفلك التي تجري في, باللغة السواحيلية

﴿إن في خلق السموات والأرض واختلاف الليل والنهار والفلك التي تجري في﴾ [البَقَرَة: 164]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika, katika kuumba mbingu kwa kuzifanya ziinuke juu na ziwe kunjufu, na ardhi kwa majabali yake, mabonde yake na bahari zake, na katika kutafautiana usiku na mchana kwa urefu na ufupi, giza na muangaza, na kuandamana kwao kwa kila mmoja kukaa pahali pa mwingine, na katika majahazi yanayopita baharini, yanayobeba vitu vinavyowanufaisha watu, na katika maji ya mvua Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, Akaipa uhai ardhi kwa maji hayo ikawa rangi ya kijani yenye kupendeza baada ya kuwa kavu isiyokuwa na mimea, na vile Alivyoeneza Mwenyezi Mungu humo kila kitambaacho juu ya ardhi hiyo, na katika yale Aliyowaneemesha kwayo ya kuugeuza upepo na kuuelekeza, na katika mawingu yanayopelekwa baina ya mbingu na ardhi, hakika, katika dalili zote hizo zilizopita, pana alama za upweke wa Mwenyezi Mungu na ukubwa wa neema Zake kwa watu wanaoelewa sehemu za hoja na wanaozifahamu dalili za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka juu ya upweke Wake na kustahiki Kwake Peke Yake kuabudiwa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek