×

Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda 2:165 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:165) ayat 165 in Swahili

2:165 Surah Al-Baqarah ayat 165 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 165 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَندَادٗا يُحِبُّونَهُمۡ كَحُبِّ ٱللَّهِۖ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَشَدُّ حُبّٗا لِّلَّهِۗ وَلَوۡ يَرَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ إِذۡ يَرَوۡنَ ٱلۡعَذَابَ أَنَّ ٱلۡقُوَّةَ لِلَّهِ جَمِيعٗا وَأَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعَذَابِ ﴾
[البَقَرَة: 165]

Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana. Na laiti walio dhulumu wakajua watakapo iona adhabu kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ومن الناس من يتخذ من دون الله أندادا يحبونهم كحب الله والذين, باللغة السواحيلية

﴿ومن الناس من يتخذ من دون الله أندادا يحبونهم كحب الله والذين﴾ [البَقَرَة: 165]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Pamoja na hizi hoja za kukata, kinatoka kikundi cha watu wakichukua, badala ya Mwenyezi Mungu, masanamu na wategemewa wakiwafanya ni kama Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kuwapa mapenzi, heshima na twaa, Mambo yasiyostahiki kufanyiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na Waumini, mapenzi yao kwa Mwenyezi Mungu ni makubwa zaidi kuliko mapenzi ya hawa makafiri kwa Mwenyezi Mungu na kwa waungu wao. Sababu Waumini wamemtakasia Mwenyezi Mungu mapenzi yao yote. Na hao makafiri wamemshirikisha Mwenyezi Mungu katika mapenzi. Na lau wangalijua wale waliojidhulumu nafsi zao kwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika maisha ya kidunia, pindi watakapoiona adhabu ya Akhera, kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Peke Yake Mwenye nguvu zote na kwamba Mwenyezi Mungu ni mkali wa adhabu, hawangaliwafanya wasiokuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni waungu wakawa wanawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, na kujikurubisha nao Kwake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek