Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 168 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ كُلُواْ مِمَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٌ ﴾
[البَقَرَة: 168]
﴿ياأيها الناس كلوا مما في الأرض حلالا طيبا ولا تتبعوا خطوات الشيطان﴾ [البَقَرَة: 168]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi watu, kuleni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, iliyoko kwenye ardhi, ile ambayo Amewahalalishia nyinyi, nayo ni iliyo tohara isiyokuwa najisi, inayonufaisha isiyodhuru wala msifuate njia za Shetani katika kuhalalisha, kuharamisha, uzushi na maasia. Hakika Yeye ni adui yenu mwenye uadui uliyo wazi |