Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 191 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوهُمۡ وَأَخۡرِجُوهُم مِّنۡ حَيۡثُ أَخۡرَجُوكُمۡۚ وَٱلۡفِتۡنَةُ أَشَدُّ مِنَ ٱلۡقَتۡلِۚ وَلَا تُقَٰتِلُوهُمۡ عِندَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَٰتِلُوكُمۡ فِيهِۖ فَإِن قَٰتَلُوكُمۡ فَٱقۡتُلُوهُمۡۗ كَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ ﴾
[البَقَرَة: 191]
﴿واقتلوهم حيث ثقفتموهم وأخرجوهم من حيث أخرجوكم والفتنة أشد من القتل ولا﴾ [البَقَرَة: 191]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na waueni wale wanaopigana na nyinyi miongoni mwa Washirikina popote mtakapowakuta, na muwtoe kutoka pahali walipowatoa, napo ni Maka. Na fitina, ambayo ni ukafiri na ushirikina na kuwazuia watu na Uislamu, ni mbaya zaidi kuliko nyinyi kuwaua wao. Wala msiwaanzie vita katika Msikiti wa Haramu, kwa kuheshimu sehemu zake tukufu, mpaka wao wawaanzie vita humo. Na iwapo watawapiga vita katika Msikiti wa Haramu, basi waueni hapo. Mfano wa malipo hayo ya kutisha yatakuwa ndiyo malipo ya Makafiri |