Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 199 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿ثُمَّ أَفِيضُواْ مِنۡ حَيۡثُ أَفَاضَ ٱلنَّاسُ وَٱسۡتَغۡفِرُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 199]
﴿ثم أفيضوا من حيث أفاض الناس واستغفروا الله إن الله غفور رحيم﴾ [البَقَرَة: 199]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na iwe kuondoka kwenu kutoka kisimamo cha Arafa, ambapo ndipo alipoondoka Ibrahim, amani imshukie, ni katika hali ya kumkhalifu, kwa hilo, yule asiyesimama hapo miongoni mwa watu wa zama za ujinga. Na muombeni Mwenyezi Mungu Awasamehe madhambi yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaghufiria waja wake waombao maghufira, wanaotubia, ni mwenye huruma kwao |