Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 198 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿لَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَبۡتَغُواْ فَضۡلٗا مِّن رَّبِّكُمۡۚ فَإِذَآ أَفَضۡتُم مِّنۡ عَرَفَٰتٖ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ عِندَ ٱلۡمَشۡعَرِ ٱلۡحَرَامِۖ وَٱذۡكُرُوهُ كَمَا هَدَىٰكُمۡ وَإِن كُنتُم مِّن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلضَّآلِّينَ ﴾
[البَقَرَة: 198]
﴿ليس عليكم جناح أن تبتغوا فضلا من ربكم فإذا أفضتم من عرفات﴾ [البَقَرَة: 198]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hapana ubaya wowote kwenu kutafuta riziki itokayo kwa Mola wenu, kwa kupata faida ya biashara, ndani ya siku za Hija.Basi mtakapo kuondoka, baada ya kutwa jua, mkirejea kutoka Arafa- napo ni pahali ambapo Mahujaji husimama siku ya tisa ya Mfungotatu-, mtajeni Mwenyezi Mungu kwa kuleta Tasbihi, Talbiyah(Labbaika Allahumma labbaika..) na dua katika sehemu tukufu ya Al- Mashcar al-Harām: Muzdalifa. Na mumtaje Mwenyezi Mungu kwa njia ya kisawa Aliyowaongoza nayo. Na mlikuwa kabla yauongofu huo mko katika upotevu, hamuijui haki |