Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 2 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿ذَٰلِكَ ٱلۡكِتَٰبُ لَا رَيۡبَۛ فِيهِۛ هُدٗى لِّلۡمُتَّقِينَ ﴾
[البَقَرَة: 2]
﴿ذلك الكتاب لا ريب فيه هدى للمتقين﴾ [البَقَرَة: 2]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Qurani hii ni kitabu kisicho na shaka kuwa kinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Haifai kwa mtu yoyote kufanya shaka juu yake kwa uwazi wake. Wananufaika kwayo wenye uchajimungu (taqwā), wenye kujikinga kwa elimu yenye manufaa na amali njema, na wao ndio wanaomuogopa Mwenyezi Mungu na kufuata hukumu Zake |