Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 21 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱعۡبُدُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ ﴾
[البَقَرَة: 21]
﴿ياأيها الناس اعبدوا ربكم الذي خلقكم والذين من قبلكم لعلكم تتقون﴾ [البَقَرَة: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwito utokao kwa Mwenyezi Mungu kwa binadamu wote: Muabuduni Mwenyezi Mungu Ambaye Amewalea kwa neema zake, na mumuogope wala msiende kinyume na dini Yake. Kwani yeye ndiye Aliyewaumba kutoka kwenye hali ya kutokuwako, na Akawaumba waliokuwa kabla yenu, ili muwe ni miongoni mwa wenye kumcha Mwenyezi Mungu ambao Yeye Ameridhika nao na wao wameridhika na Yeye |