Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 216 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِتَالُ وَهُوَ كُرۡهٞ لَّكُمۡۖ وَعَسَىٰٓ أَن تَكۡرَهُواْ شَيۡـٔٗا وَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَعَسَىٰٓ أَن تُحِبُّواْ شَيۡـٔٗا وَهُوَ شَرّٞ لَّكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ ﴾
[البَقَرَة: 216]
﴿كتب عليكم القتال وهو كره لكم وعسى أن تكرهوا شيئا وهو خير﴾ [البَقَرَة: 216]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Amewafaradhia, enyi Waumini, kupigana na Makafiri, hali ya kuwa ni jambo lenye kuchukiwa na nyinyi kimaumbile, kwa uzito wake na hatari zake nyingi. Na huenda mkakichukia kitu nacho, kwa uhakika wake, ni kheri kwenu. Na huenda mkakipenda kitu kwa ajili ya raha na ladha za karibu zilizomo, nacho, kwa uhakika wake, ni shari kwenu. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Analijua lenye kheri kwenu, na nyinyi hamlijui hilo. Kwa hivyo harakisheni kupigana jihadi katika njia Yake |