×

Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati 2:217 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:217) ayat 217 in Swahili

2:217 Surah Al-Baqarah ayat 217 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 217 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلشَّهۡرِ ٱلۡحَرَامِ قِتَالٖ فِيهِۖ قُلۡ قِتَالٞ فِيهِ كَبِيرٞۚ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَكُفۡرُۢ بِهِۦ وَٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ وَإِخۡرَاجُ أَهۡلِهِۦ مِنۡهُ أَكۡبَرُ عِندَ ٱللَّهِۚ وَٱلۡفِتۡنَةُ أَكۡبَرُ مِنَ ٱلۡقَتۡلِۗ وَلَا يَزَالُونَ يُقَٰتِلُونَكُمۡ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمۡ عَن دِينِكُمۡ إِنِ ٱسۡتَطَٰعُواْۚ وَمَن يَرۡتَدِدۡ مِنكُمۡ عَن دِينِهِۦ فَيَمُتۡ وَهُوَ كَافِرٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ﴾
[البَقَرَة: 217]

Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa. Lakini kuzuilia watu wasende katika Njia ya Mwenyezi Mungu na kumkanusha Yeye, na kuzuilia watu wasende kwenye Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wake humo, ni makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza. Na yeyote katika nyinyi akiacha Dini yake akafa naye ni kafiri, basi hao ndio ambao a'mali zao zimeharibika duniani na Akhera. Na hao ndio watu wa Motoni; humo watadumu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: يسألونك عن الشهر الحرام قتال فيه قل قتال فيه كبير وصد عن, باللغة السواحيلية

﴿يسألونك عن الشهر الحرام قتال فيه قل قتال فيه كبير وصد عن﴾ [البَقَرَة: 217]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wanakuuliza washirikina, ewe Mtume, kuhusu mwezi mtukufu wa Haram, «Inafaa kupigana ndani yake?» Waambie, «Kupigana katika mwezi mtukufu wa Ḥarām ni jambo kubwa kwa Mwenyezi Mungu kuuhalalisha na kumwaga damu ndani yake. Na kuwazuia kwenu watu kuingia katika Uislamu, kwa kuwaadhibu na kuwatisha na kumkanusha kwenu Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na dini Yake, na kuwzuia Waislamu wasiingie kwenye Msikiti wa Haram, na kumtoa Nabii na waliogura naye kutoka huko, ambao wao ndiwo wakazi na wasimamizi wake, hilo ni dhambi kubwa mno na nikosa kubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuliko kupigana katika mwezi mtukufu wa Haram. Na ushirikina mlionao ni jambo kubwa zaidi na baya zaidi kuliko kuua katika mwezi mtukufu wa Haram. Na Makafiri hawa hawatatishika na kukomeka na makosa yao, bali wao ni wenye kuendelea nayo. Wala hawataacha kuwapiga vita mpaka wawatoe kwenye Uislamu kuwatia kwenye ukafiri, iwapo wataweza kulihakikisha hilo. Na mwenye kuwatii wao, kati yenu, enyi Waislamu, akaacha dini yake na akafa katika ukafiri, basi amali zake zitapotea duniani na Akhera na atakuwa ni miongoni mwa watakaodumu kwenye moto wa Jahanamu, hatatoka humo milele
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek