×

Na wanawake walio achwa wangoje peke yao mpaka t'ahara (au hedhi) tatu 2:228 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:228) ayat 228 in Swahili

2:228 Surah Al-Baqarah ayat 228 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 228 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿وَٱلۡمُطَلَّقَٰتُ يَتَرَبَّصۡنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَٰثَةَ قُرُوٓءٖۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكۡتُمۡنَ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ فِيٓ أَرۡحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤۡمِنَّ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنۡ أَرَادُوٓاْ إِصۡلَٰحٗاۚ وَلَهُنَّ مِثۡلُ ٱلَّذِي عَلَيۡهِنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيۡهِنَّ دَرَجَةٞۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴾
[البَقَرَة: 228]

Na wanawake walio achwa wangoje peke yao mpaka t'ahara (au hedhi) tatu zipite. Wala haiwajuzii kuficha alicho umba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya sulhu. Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima

❮ Previous Next ❯

ترجمة: والمطلقات يتربصن بأنفسهن ثلاثة قروء ولا يحل لهن أن يكتمن ما خلق, باللغة السواحيلية

﴿والمطلقات يتربصن بأنفسهن ثلاثة قروء ولا يحل لهن أن يكتمن ما خلق﴾ [البَقَرَة: 228]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na wanawake waliotalikiwa, waingiao hedhini, itawalazimu kungojea bila kuolewa muda wa twahara tatu au hedhi tatu baada ya kutalikiwa. Kukaa kwao kipindi hicho cha eda ni ili wahakikishe kuwa uzao ni safi, hawana mamba. Wala haifai kuolewa na mume mwengine katika kipindi hicho mpaka kiishe. Wala si halali kwao kukificha kile Alichokiumba Mwenyezi Mungu katika zao zao miongoni mwa mimba au hedhi, iwapo hao wanawake walioachwa ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kikweli. Na waume wa wale waliotalikiwa wana haki ya kuwarejea wake zao hao iwapo bado wamo kwenye maeda yao. Na hilo la kuwarejea inapasa liwe ni kwa lengo la kheri na kutengeneza, wala lisiwe ni kwa lengo la kuwadhuru na kuwatesa kwa kulirefusha eda. Na wanawake wana haki kwa waume zao kama waume walivyo na haki kwa wake zao, kwa njia ya wema. Na wanaume kwa wake zao wana cheo cha zaidi kwa kukaa nao kwa uzuri, kutangamana nao kwa wema, kusimamia nyumba na kwamba talaka iko mikononi mwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mshindi, Ana enzi na uwezo wa kutendesha nguvu, ni Mwingi wa hekima, Huweka kila kitu mahali pake panapalingana
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek