×

Basi Taluti alipo ondoka na majeshi alisema: Mwenyezi Mungu atakujaribuni kwa mto. 2:249 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:249) ayat 249 in Swahili

2:249 Surah Al-Baqarah ayat 249 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 249 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِٱلۡجُنُودِ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ مُبۡتَلِيكُم بِنَهَرٖ فَمَن شَرِبَ مِنۡهُ فَلَيۡسَ مِنِّي وَمَن لَّمۡ يَطۡعَمۡهُ فَإِنَّهُۥ مِنِّيٓ إِلَّا مَنِ ٱغۡتَرَفَ غُرۡفَةَۢ بِيَدِهِۦۚ فَشَرِبُواْ مِنۡهُ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُۥ هُوَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ قَالُواْ لَا طَاقَةَ لَنَا ٱلۡيَوۡمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦۚ قَالَ ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ ٱللَّهِ كَم مِّن فِئَةٖ قَلِيلَةٍ غَلَبَتۡ فِئَةٗ كَثِيرَةَۢ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ ﴾
[البَقَرَة: 249]

Basi Taluti alipo ondoka na majeshi alisema: Mwenyezi Mungu atakujaribuni kwa mto. Atakaye kunywa humo si pamoja nami, na asiye kunywa atakuwa pamoja nami: ila atakaye teka kiasi ya kitanga cha mkono wake. Lakini walikunywa humo isipo kuwa wachache tu miongoni mwao. Alipo vuka mto yeye na wale walio amini pamoja naye, walisema: Leo hatumwezi Jaluti (Goliati) na majeshi yake. Wakasema wale wenye yakini ya kukutana na Mwenyezi Mungu: Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri

❮ Previous Next ❯

ترجمة: فلما فصل طالوت بالجنود قال إن الله مبتليكم بنهر فمن شرب منه, باللغة السواحيلية

﴿فلما فصل طالوت بالجنود قال إن الله مبتليكم بنهر فمن شرب منه﴾ [البَقَرَة: 249]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Alipotoka Twalut na askari wake kwenda kupigana na watu majabari, aliwaambia, «Mwenyezi Mungu Atawapa mtihani wa subira kwa mto uliyo mbele yenu mtakaouvuka, ili abainike mwenye Imani na aliye mnafiki. Yoyote kati yenu atakaye kunywa maji ya mto huo, si katika mimi, wala hafai kuwa na mimi kwenye jihadi. Na yule ambaye hatayaonja maji hayo, yeye ni katika mimi, kwa kutii amri yangu, na anafaa kwa jihadi. Isipokuwa aliyeruhusiwa na akateka mteko mmoja kwa mkono wake, huyo hana lawama. Basi walipofika mtoni, waliyaangukia maji na waliyanywa sana isipokuwa idadi ya watu wachache kati yao, walisubiri juu ya kiu na joto na wakatosheka na mteko wa mkono. Wakati huo wale walioasi amri, walirudi nyuma. Tālūt pamoja na wale Waumini wachache walipouvuka mto - walikuwa watu zaidi ya mia tatu na kumi- kwa ajili ya kupambana na maadui zao na wakaona wingi wa maadui zao na wingi wa silaha walionazo, walisema, «Hatuna uwezo leo wa kupigana na Jālūt na askari wake wenye nguvu. Hapo, wale wliokuwa na yakini ya kukutana na Mola Wao walijibu wakiwakumbusha ndugu zao juu ya Mwenyezi Mungu na uwezo Wake, «Nivikundi vingapi vichache, venye imani na subira, viliyashinda, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, makundi yaliyokuwa na watu wengi makafiri wenye kuasi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Yupo pamoja na wenye subira kwa taufiki Yake na nusra Yake na malipo Yake mema
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek