Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 250 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿وَلَمَّا بَرَزُواْ لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦ قَالُواْ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَيۡنَا صَبۡرٗا وَثَبِّتۡ أَقۡدَامَنَا وَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ ﴾
[البَقَرَة: 250]
﴿ولما برزوا لجالوت وجنوده قالوا ربنا أفرغ علينا صبرا وثبت أقدامنا وانصرنا﴾ [البَقَرَة: 250]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na walipojitokeza kwa Jālūt na askari wake na wakaiona hatari kwa macho yao, walifazaika na kumuelekea kwa Mwenyezi Mungu kwa maombi na kunyenyekea huku wakisema, «EweMola wetu! Tumiminie subira nyingi kwenye nyoyo zetu, Uzithibitishe nyayo zetu ziwe thabiti muda wa kupigana na adui, zisiwe na uoga wa kukimbia vita, na Utunusuru kwa msaada wako juu ya watu makafiri |