Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 266 - البَقَرَة - Page - Juz 3
﴿أَيَوَدُّ أَحَدُكُمۡ أَن تَكُونَ لَهُۥ جَنَّةٞ مِّن نَّخِيلٖ وَأَعۡنَابٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ لَهُۥ فِيهَا مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ وَأَصَابَهُ ٱلۡكِبَرُ وَلَهُۥ ذُرِّيَّةٞ ضُعَفَآءُ فَأَصَابَهَآ إِعۡصَارٞ فِيهِ نَارٞ فَٱحۡتَرَقَتۡۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَتَفَكَّرُونَ ﴾
[البَقَرَة: 266]
﴿أيود أحدكم أن تكون له جنة من نخيل وأعناب تجري من تحتها﴾ [البَقَرَة: 266]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je anapendelea mmoja wenu awe na bustani yenye mitende na mizabibu, ambayo inapita chini ya miti yake maji tamu, na ndani yake ana kila aina ya matunda, na amefikia hali ya ukongwe ya kutoweza kupanda mimea kama hii, na ana watoto wadogo wanaohitaji bustani hii, na katika hali hii ukavuma upepo mkali uchomao, ukaja ukaiteketeza? Hivi ndivyo hali ya wasio na ikhlasi kataka utoaji wao; watakuja Siku ya Kiyama na hawana jema lolote lao. Kwa ufafanuzi huu, Mwenyezi Mungu Anawabainishia mambo yanayowafaa nyinyi, ili mtaamali na kumtakasia Mwenyezi Mungu utoaji wenu |