Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 265 - البَقَرَة - Page - Juz 3
﴿وَمَثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمُ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِ وَتَثۡبِيتٗا مِّنۡ أَنفُسِهِمۡ كَمَثَلِ جَنَّةِۭ بِرَبۡوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٞ فَـَٔاتَتۡ أُكُلَهَا ضِعۡفَيۡنِ فَإِن لَّمۡ يُصِبۡهَا وَابِلٞ فَطَلّٞۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ ﴾
[البَقَرَة: 265]
﴿ومثل الذين ينفقون أموالهم ابتغاء مرضات الله وتثبيتا من أنفسهم كمثل جنة﴾ [البَقَرَة: 265]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mfano wa wale ambao wanatoa mali yao kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kwa kuwa na itikadi iliyojikita ya kuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, ni kama mfano wa bustani kubwa iliyoko kwenye ardhi ya juu iliyo nzuri iliyonyeshewa na mvua nyingi, yakaongezeka kwa wingi matunda yake. Na hata kama haingalinyeshewa na mvua nyingi, rasharasha la mvua lingalitosha kuifanya itoe ongezeko lingi la matunda. Basi hivyo ndivyo ulivyo utoaji wa watu wenye ikhlasi; amali zao zinakubaliwa mbele ya Mwenyezi Mungu na kuongezwa, ziwe ni chache au ni nyingi. Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuchungulia siri, Ndiye Mwenye kuyaona ya nje na ya ndani, Anampa thawabu kila mtu kulingana na ikhlasi yake |