Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 267 - البَقَرَة - Page - Juz 3
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنفِقُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا كَسَبۡتُمۡ وَمِمَّآ أَخۡرَجۡنَا لَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِۖ وَلَا تَيَمَّمُواْ ٱلۡخَبِيثَ مِنۡهُ تُنفِقُونَ وَلَسۡتُم بِـَٔاخِذِيهِ إِلَّآ أَن تُغۡمِضُواْ فِيهِۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴾
[البَقَرَة: 267]
﴿ياأيها الذين آمنوا أنفقوا من طيبات ما كسبتم ومما أخرجنا لكم من﴾ [البَقَرَة: 267]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mlioniamini na mkawafuata Mitume wangu, toeni miongoni mwa halali mliyoichuma na ile tuliyowatolea kutoka kwenye ardhi. Na wala msikusudie kutoa kibaya, katika hiyo halali, kuwapa mafukara, ambacho lau nyinyi mngalipewa, hamngalikipokea isipokuwa mkiwa mtapuuza ubaya na upungufu ulionacho. Ni vipi nyinyi mnaridhika kumpa Mwenyezi Mungu kitu ambacho hamridhiki nacho mkipewa? Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu Aliyewaruzuku Anajitosha kutohitajia sadaka zenu, ni Mstahiki wa kusifiwa na Mhimidiwa kwa kila hali |