Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 281 - البَقَرَة - Page - Juz 3
﴿وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا تُرۡجَعُونَ فِيهِ إِلَى ٱللَّهِۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ ﴾
[البَقَرَة: 281]
﴿واتقوا يوما ترجعون فيه إلى الله ثم توفى كل نفس ما كسبت﴾ [البَقَرَة: 281]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na itahadharini, enyi watu, Siku matakaporejeshwa kwa Mwenyezi Mungu, nayo ni Siku ya Kiyama, mtakapo kuorodheshwa kwa Mwenyezi Mungu ili Awahesabu na Amlipe kila mmoja miongoni mwenu kwa alilolitenda la kheri au la shari bila ya kufikiwa na maonevu. Katika aya hii pana ishara kwamba kujiepusha na mapato ya riba yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, ni kukamilisha Imani na haki za Imani za kutekeleza Swala, kutoa Zaka na kufanya amali njema |