×

Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi 2:30 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:30) ayat 30 in Swahili

2:30 Surah Al-Baqarah ayat 30 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 30 - البَقَرَة - Page - Juz 1

﴿وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِنِّي جَاعِلٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ خَلِيفَةٗۖ قَالُوٓاْ أَتَجۡعَلُ فِيهَا مَن يُفۡسِدُ فِيهَا وَيَسۡفِكُ ٱلدِّمَآءَ وَنَحۡنُ نُسَبِّحُ بِحَمۡدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَۖ قَالَ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ ﴾
[البَقَرَة: 30]

Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وإذ قال ربك للملائكة إني جاعل في الأرض خليفة قالوا أتجعل فيها, باللغة السواحيلية

﴿وإذ قال ربك للملائكة إني جاعل في الأرض خليفة قالوا أتجعل فيها﴾ [البَقَرَة: 30]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kumbuka, ewe Mtume, Aliposema Mola wako kuwaambia Malaika, “Mimi nitawaweka watu kwenye ardhi, ili waiimarishe kwa kupishana: wakiondoka watu watakuja wengine baada yao.” Wakasema, “Ewe Mola wetu! Tufundishe na utuongoze, ni kwa hekima gani kuwaumba hawa, pamoja na kuwa mambo yao yatakuwa ni kuleta uharibifu katika ardhi na kumwaga damu kwa dhulma na uonevu, na hali sisi tuko chini ya amri yako: tunakuepusha na mabaya maepusho yanayonasibiana na Sifa zako njema na utukufu Wako, na tunakusifu kwa kila sifa za ukamilifu na utukufu?” Mwenyezi Mungu Akasema kuwaambia, “Mimi najua msiyoyajua kuhusu uzito wa maslahi katika kuwaumba wao.”
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek