Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 71 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٞ لَّا ذَلُولٞ تُثِيرُ ٱلۡأَرۡضَ وَلَا تَسۡقِي ٱلۡحَرۡثَ مُسَلَّمَةٞ لَّا شِيَةَ فِيهَاۚ قَالُواْ ٱلۡـَٰٔنَ جِئۡتَ بِٱلۡحَقِّۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُواْ يَفۡعَلُونَ ﴾
[البَقَرَة: 71]
﴿قال إنه يقول إنها بقرة لا ذلول تثير الأرض ولا تسقي الحرث﴾ [البَقَرَة: 71]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mūsā aliwaambia, “Mwenyezi Mungu Anasema kwamba huyo ni ng’ombe asiyetumiwa kwa kazi ya kulima ardhi ya kilimo, hakutayarishwa kutia maji, hana kasoro yoyote na hana alama yoyote ya rangi isiyokuwa rangi ya ngozi yake.” Wakasema, “Sasa umekuja na ukweli wa sifa ya ng’ombe.” Wakalazimika kumchinja baada ya muda mrefu wa mbinu za kuchelewesha. Na walikuwa karibu kutofanya hilo kwa ushindani wao. Hivi ndivyo walivyojitilia mkazo, ndipo Mwenyezi Mungu Akawafanyia mkazo |