Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 73 - البَقَرَة - Page - Juz 1
﴿فَقُلۡنَا ٱضۡرِبُوهُ بِبَعۡضِهَاۚ كَذَٰلِكَ يُحۡيِ ٱللَّهُ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَيُرِيكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ ﴾
[البَقَرَة: 73]
﴿فقلنا اضربوه ببعضها كذلك يحي الله الموتى ويريكم آياته لعلكم تعقلون﴾ [البَقَرَة: 73]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Tukasema, “Mpigeni aliyeuliwa kwa sehemu ya yule ng’ombe aliyechinjwa, Mwenyezi Mungu atamfufua akiwa hai na atawaambia muuaji wake ni nani.” Basi wakampiga kwa ile sehemu ya ng’ombe, Mwenyezi Mungu Akamhuisha na akamtaja muuaji wake. Hivyo ndivyo Anavyohuisha Mwenyezi Mungu wafu Siku ya Kiyama na kuwaonyesha nyinyi, Wana wa Isrāīl, miujiza Yake yenye dalili ya ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, ili mfikiri kwa akili zenu mpate kujiepusha na vitendo vya kumuasi |