×

Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe 2:74 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:74) ayat 74 in Swahili

2:74 Surah Al-Baqarah ayat 74 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 74 - البَقَرَة - Page - Juz 1

﴿ثُمَّ قَسَتۡ قُلُوبُكُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَٱلۡحِجَارَةِ أَوۡ أَشَدُّ قَسۡوَةٗۚ وَإِنَّ مِنَ ٱلۡحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنۡهُ ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ وَإِنَّ مِنۡهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخۡرُجُ مِنۡهُ ٱلۡمَآءُۚ وَإِنَّ مِنۡهَا لَمَا يَهۡبِطُ مِنۡ خَشۡيَةِ ٱللَّهِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ ﴾
[البَقَرَة: 74]

Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe yanayo timbuka mito, na kuna mengine yanayo pasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya khofu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yafanya

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ثم قست قلوبكم من بعد ذلك فهي كالحجارة أو أشد قسوة وإن, باللغة السواحيلية

﴿ثم قست قلوبكم من بعد ذلك فهي كالحجارة أو أشد قسوة وإن﴾ [البَقَرَة: 74]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Lakini nyinyi hamkufaidika na hilo. Kwani baada ya miujiza yote hii yenye kupita mipaka ya uwezo wa kiumbe, nyoyo zenu zilikuwa ngumu na shupavu kwa namna ambayo hakuna kheri iliopenyeza ndani, na hazikulainika mbele ya miujiza yenye kushinda niliyowaonesha, mpaka nyoyo zenu zikafikia hadi ya kuwa ni kama jiwe gumu, bali zililishinda jiwe kwa ugumu wake. Kwani miongoni mwa mawe kuna yanayopanuka na kutoboka na maji yakabubujika kwa wingi kutoka humo mpaka yakawa ni mito yenye kupata. Na miongoni mwayo kuna yanayofanya nyufa, yakapasuka na kuchimbuka maji ya chemchemi na mikondo. Na miongoni mwayo kuna yanayoanguka kutoka juu ya milima kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kumuadhimisha. Na Mwenyezi Mungu Hakuwa ni Mwenye kughafilika kwa mnayoyafanya
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek