×

Dada yako alipo kwenda na akasema: Je! Nikujuulisheni mtu wa kuweza kumlea? 20:40 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Ta-Ha ⮕ (20:40) ayat 40 in Swahili

20:40 Surah Ta-Ha ayat 40 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Ta-Ha ayat 40 - طه - Page - Juz 16

﴿إِذۡ تَمۡشِيٓ أُخۡتُكَ فَتَقُولُ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ مَن يَكۡفُلُهُۥۖ فَرَجَعۡنَٰكَ إِلَىٰٓ أُمِّكَ كَيۡ تَقَرَّ عَيۡنُهَا وَلَا تَحۡزَنَۚ وَقَتَلۡتَ نَفۡسٗا فَنَجَّيۡنَٰكَ مِنَ ٱلۡغَمِّ وَفَتَنَّٰكَ فُتُونٗاۚ فَلَبِثۡتَ سِنِينَ فِيٓ أَهۡلِ مَدۡيَنَ ثُمَّ جِئۡتَ عَلَىٰ قَدَرٖ يَٰمُوسَىٰ ﴾
[طه: 40]

Dada yako alipo kwenda na akasema: Je! Nikujuulisheni mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ulimuuwa mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi. Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kama ilivyo kadiriwa, ewe Musa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إذ تمشي أختك فتقول هل أدلكم على من يكفله فرجعناك إلى أمك, باللغة السواحيلية

﴿إذ تمشي أختك فتقول هل أدلكم على من يكفله فرجعناك إلى أمك﴾ [طه: 40]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
«Na pia tulikuneemesha pindi alipokwenda dadako kufuatilia mambo yako, kisha akasema akiwaambia waliokuchukua, ‘Je, niwajulishe nyinyi yule anayeweza kuwalelea na kuwanyonyeshea?’ Basi tukakurudisha kwa mamako baada ya kwamba ulikuwa kwenye mikono ya Fir'awn ili nafsi yake itulie kwa kuokoka kwako na kuzama na kuuawa na asiwe na masikitiko ya kukukosa. Na ulimuua mtu wa kabila la Kibti kimakosa tukakuokoa na makero ya kitendo chako hiko na kuogopa kuuawa. Na tulikuonja maonjo mengi, ukatoka kwa kuogopa ukaenda kwa watu wa Madyan, ukaketi kwao miaka mingi, kisha ukaja kutoka Madyan katika kipindi tulichokipanga kwa kukutumiliza, kuja kulikofikiana na mpango wa Mwenyezi Mungu na matakwa Yake. Na mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu Mwingi wa baraka Aliyetukuka
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek