Quran with Swahili translation - Surah Ta-Ha ayat 90 - طه - Page - Juz 16
﴿وَلَقَدۡ قَالَ لَهُمۡ هَٰرُونُ مِن قَبۡلُ يَٰقَوۡمِ إِنَّمَا فُتِنتُم بِهِۦۖ وَإِنَّ رَبَّكُمُ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَٱتَّبِعُونِي وَأَطِيعُوٓاْ أَمۡرِي ﴾
[طه: 90]
﴿ولقد قال لهم هارون من قبل ياقوم إنما فتنتم به وإن ربكم﴾ [طه: 90]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa kweli, Hārūn aliwaambia Wana wa Isrāīl kabla Mūsā hajarudi kuwajia, «Enyi watu wangu, hakika nyinyi mumetahiniwa na huyu kigombe, ili aonekana wazi mwenye Imani miongoni mwenu apate kujitenga na mwenye kukanusha. Kwa hakika Mola wenu ni Al-Rahmān (Mwingi wa Rehema) si mwingine. Basi nifuateni katika lile ninalowaitia la kumuabudu Mwenyezi Mungu na muitii amri yangu katika kufuata sheria Yake.» |