Quran with Swahili translation - Surah Al-Anbiya’ ayat 50 - الأنبيَاء - Page - Juz 17
﴿وَهَٰذَا ذِكۡرٞ مُّبَارَكٌ أَنزَلۡنَٰهُۚ أَفَأَنتُمۡ لَهُۥ مُنكِرُونَ ﴾
[الأنبيَاء: 50]
﴿وهذا ذكر مبارك أنـزلناه أفأنتم له منكرون﴾ [الأنبيَاء: 50]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hii Qur’ani ambayo Mwenyezi Mungu Ameiteremsha kwa Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukliye, ni ukumbusho kwa anayejikumbusha nayo na akatekeleza amri Zake na akajiepusha na makatazo Yake, ina kheri nyingi na manufaa makubwa. Je, mnaikanusha na hali ina upeo wa uwazi na ufunuzi |