Quran with Swahili translation - Surah Al-Anbiya’ ayat 90 - الأنبيَاء - Page - Juz 17
﴿فَٱسۡتَجَبۡنَا لَهُۥ وَوَهَبۡنَا لَهُۥ يَحۡيَىٰ وَأَصۡلَحۡنَا لَهُۥ زَوۡجَهُۥٓۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡخَيۡرَٰتِ وَيَدۡعُونَنَا رَغَبٗا وَرَهَبٗاۖ وَكَانُواْ لَنَا خَٰشِعِينَ ﴾
[الأنبيَاء: 90]
﴿فاستجبنا له ووهبنا له يحيى وأصلحنا له زوجه إنهم كانوا يسارعون في﴾ [الأنبيَاء: 90]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Tukamkubalia maombi yake na tukamtunuku yeye, akiwa katika hali ya uzee, mwanawe Yaḥyā, na tukamfanya mke wake ni mwema wa tabia na ni mwenye kufaa kushika mimba na kuzaa baada ya kuwa tasa. Kwa kweli, wao walikuwa wakiikimbilia kila kheri, na wakituomba wakitumai kupata mazuri yaliyoko kwetu wakiogopa mateso yetu na walikuwa wadhalilifu na wanyonge kwetu |