Quran with Swahili translation - Surah Al-Anbiya’ ayat 89 - الأنبيَاء - Page - Juz 17
﴿وَزَكَرِيَّآ إِذۡ نَادَىٰ رَبَّهُۥ رَبِّ لَا تَذَرۡنِي فَرۡدٗا وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡوَٰرِثِينَ ﴾
[الأنبيَاء: 89]
﴿وزكريا إذ نادى ربه رب لا تذرني فردا وأنت خير الوارثين﴾ [الأنبيَاء: 89]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka, ewe Mtume, kisa cha mja wa Mwenyezi Mungu Zakariyya alipomuomba Mola wake Amtunukie wana, wakati umri wake ulipokuwa mkubwa, kwa kusema, «Mola wangu! Usiniache pweke ni siwe na mwana! Basi nitunuku mrithi wa kusimamia mambo ya Dini kwa watu baada yangu mimi, na wewe Ndiye bora wa wenye kusalia na bora wa wenye kusimamia mambo yangu baada yangu kwa uzuri!» |