×

Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola 22:40 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-hajj ⮕ (22:40) ayat 40 in Swahili

22:40 Surah Al-hajj ayat 40 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 40 - الحج - Page - Juz 17

﴿ٱلَّذِينَ أُخۡرِجُواْ مِن دِيَٰرِهِم بِغَيۡرِ حَقٍّ إِلَّآ أَن يَقُولُواْ رَبُّنَا ٱللَّهُۗ وَلَوۡلَا دَفۡعُ ٱللَّهِ ٱلنَّاسَ بَعۡضَهُم بِبَعۡضٖ لَّهُدِّمَتۡ صَوَٰمِعُ وَبِيَعٞ وَصَلَوَٰتٞ وَمَسَٰجِدُ يُذۡكَرُ فِيهَا ٱسۡمُ ٱللَّهِ كَثِيرٗاۗ وَلَيَنصُرَنَّ ٱللَّهُ مَن يَنصُرُهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴾
[الحج: 40]

Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: الذين أخرجوا من ديارهم بغير حق إلا أن يقولوا ربنا الله ولولا, باللغة السواحيلية

﴿الذين أخرجوا من ديارهم بغير حق إلا أن يقولوا ربنا الله ولولا﴾ [الحج: 40]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wale ambao walilazimishwa kutoka majumbani mwao, si kwa lolote isipokuwa ni kwa kuwa wamesilimu na wamesema, «Mola wetu ni Mwenyezi Mngu Peke Yake.» Na lau si mpango Aliouiweka Mwenyezi Mungu wa kuondoa maonevu ambayo kwayo wananufaika watu wa dini zote zilizoteremshwa na kuurudisha ubatilifu kwa kuruhusu kupigana, haki ingalishindwa katika kila ummah, ardhi ingaliharibiwa, sehemu za ibada zingalivunjwa, miongoni mwa mindule ya watawa, makanisa ya Wanaswara, majumba ya ibada ya Mayahudi na misikiti ya Waislamu ambayo Wanaswali ndani yake, na wanamtaja Mwenyezi Mungu humo kwa wingi. Na mwenye kufanya bidii kuitetea Dini ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Atamnusuru juu ya adui yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Asiyeshindwa, ni Mshindi Asiyefikiwa, Amewatendesha nguvu viumbe na Amezishika paa za nyuso zao
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek