Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 39 - الحج - Page - Juz 17
﴿أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَٰتَلُونَ بِأَنَّهُمۡ ظُلِمُواْۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ نَصۡرِهِمۡ لَقَدِيرٌ ﴾
[الحج: 39]
﴿أذن للذين يقاتلون بأنهم ظلموا وإن الله على نصرهم لقدير﴾ [الحج: 39]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Waislamu, mwanzo wao, walikuwa wamekatazwa kupigana na makafiri, wameamrishwa kuvumilia maudhi yao. Maudhi ya washirikina yalipofikia upeo wake na Mtume akatoka Makkah hali ya kugura kwenda Madina na Uislamu ukawa na nguvu, Mwenyezi Mungu Aliwaruhusu Waislamu kupigana kwa sababu hiyo ya maonevu yaliyowashukia na uadui. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwanusuru na kuwadhalilisha maadui wao |