Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 62 - الحج - Page - Juz 17
﴿ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ هُوَ ٱلۡبَٰطِلُ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡكَبِيرُ ﴾
[الحج: 62]
﴿ذلك بأن الله هو الحق وأن ما يدعون من دونه هو الباطل﴾ [الحج: 62]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hayo ni kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki Ambaye hapana yoyote Anayepasa aabudiwe isipokuwa Yeye na kwamba vile wanavyoviabudu washirikina miongoni mwa masanamu na waungu-bandia wanaodaiwa kufanana na Yeye ndio batili wasionufaisha wala kudhuru, na kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Aliye juu ya viumbe vyake kwa dhati, cheo na utendeshaji nguvu, Ndiye Aliyejiepusha na wanaodaiwa kufanana na Yeye na kuwa wendani Wake, Aliye Mkuu katika dhati Yake, majina Yake na sifa Zake. Yeye ni Mkubwa kuliko kila kitu |