Quran with Swahili translation - Surah Al-hajj ayat 67 - الحج - Page - Juz 17
﴿لِّكُلِّ أُمَّةٖ جَعَلۡنَا مَنسَكًا هُمۡ نَاسِكُوهُۖ فَلَا يُنَٰزِعُنَّكَ فِي ٱلۡأَمۡرِۚ وَٱدۡعُ إِلَىٰ رَبِّكَۖ إِنَّكَ لَعَلَىٰ هُدٗى مُّسۡتَقِيمٖ ﴾
[الحج: 67]
﴿لكل أمة جعلنا منسكا هم ناسكوه فلا ينازعنك في الأمر وادع إلى﴾ [الحج: 67]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kila watu miongoni mwa jinsi za watu waliopita tumewaekea sheria na ibada tuliowaamrisha wao kwazo, na wao ni wenye kuzitumia, basi wasikufanyie ushindani, ewe Mtume, hao washirikina wa Kikureshi kuhusu Sheria yako na yale Aliyokuamrisha Mwenyezi Mungu katika matendo ya Hija na aina zote za ibada. Na ulinganie kwenye kumpwekesha Mola wako na kumtakasia ibada na kufuata amri Yake. Hakika wewe uko kwenye Dini iliyolingana sawa, isiyokuwa na mapindi |