Quran with Swahili translation - Surah Al-Mu’minun ayat 44 - المؤمنُون - Page - Juz 18
﴿ثُمَّ أَرۡسَلۡنَا رُسُلَنَا تَتۡرَاۖ كُلَّ مَا جَآءَ أُمَّةٗ رَّسُولُهَا كَذَّبُوهُۖ فَأَتۡبَعۡنَا بَعۡضَهُم بَعۡضٗا وَجَعَلۡنَٰهُمۡ أَحَادِيثَۚ فَبُعۡدٗا لِّقَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ ﴾
[المؤمنُون: 44]
﴿ثم أرسلنا رسلنا تترى كل ما جاء أمة رسولها كذبوه فأتبعنا بعضهم﴾ [المؤمنُون: 44]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kisha tukawapeleka Mitume wetu waende kwa ummah hao, wakifuatana: hawa baada wengine. Na kila Mtume akiwalingania watu wake, wanamkanusha. Basi tukawafuatisha, kundi baada ya kundi, kwa kuwaangamiza na kuwamaliza, na hakuna kilichosalia isipokuwa ni habari za kuangamia kwao.Na tukazifanya habari hizo ni maneno ya kuzungumzwa na watu waliokuja baada yao, wakizichukuwa kuwa ni mazingatio. Basi maangamivu na kuepushwa na kila kheri ni kwa watu wasiowaamini Mitume wala kuwatii |