×

Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfano wa Nuru yake 24:35 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nur ⮕ (24:35) ayat 35 in Swahili

24:35 Surah An-Nur ayat 35 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 35 - النور - Page - Juz 18

﴿۞ ٱللَّهُ نُورُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ مَثَلُ نُورِهِۦ كَمِشۡكَوٰةٖ فِيهَا مِصۡبَاحٌۖ ٱلۡمِصۡبَاحُ فِي زُجَاجَةٍۖ ٱلزُّجَاجَةُ كَأَنَّهَا كَوۡكَبٞ دُرِّيّٞ يُوقَدُ مِن شَجَرَةٖ مُّبَٰرَكَةٖ زَيۡتُونَةٖ لَّا شَرۡقِيَّةٖ وَلَا غَرۡبِيَّةٖ يَكَادُ زَيۡتُهَا يُضِيٓءُ وَلَوۡ لَمۡ تَمۡسَسۡهُ نَارٞۚ نُّورٌ عَلَىٰ نُورٖۚ يَهۡدِي ٱللَّهُ لِنُورِهِۦ مَن يَشَآءُۚ وَيَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡأَمۡثَٰلَ لِلنَّاسِۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ ﴾
[النور: 35]

Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa ile imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa kwa mafuta yanayo toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa - Nuru juu ya Nuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: الله نور السموات والأرض مثل نوره كمشكاة فيها مصباح المصباح في زجاجة, باللغة السواحيلية

﴿الله نور السموات والأرض مثل نوره كمشكاة فيها مصباح المصباح في زجاجة﴾ [النور: 35]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu ni Nuru ya mbinguni na ardhini, Anaendesha mambo humo na Anawaongoza watu wake. Kwa hivyo, Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ni Nuru, na pazia Yake ni Nuru. Kwayo zimeng’ara mbingu na ardhi na vilivyomo ndani. Na kitabu cha Mwenyezi Mungu na uongofu wake ni nuru kutoka Kwake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake. Na lau si nuru Yake yeye Aliyetukuka, lingalishikamana giza na kupandana, hili juu ya lingine. Mfano wa nuru Yake ambayo inaongoza kupeleka Kwake, nayo ni Imani na Qura’ni ndani ya moyo wa mwenye kuamini, ni kama kishubaki, nacho ni kidirisha ukutani kisichoonyesha upande wa pili, kwenye kidirisha kuna taa, ambapo hapo kidirisha kinakusanya nuru ya ile taa, zote zikawa mwangaza wake ni mmoja. Na taa hiyo iko kwenye kiyoo, kama kawamba kiyoo hiko kwa usafi wake ni nyota ing’arao kama duri. Taa hiyo inawashwa kwa mafuta ya mti uliobarikiwa, nao ni mzaituni, si wa upande wa mashariki tu usiopatwa na jua mwisho wa mchana, wala si wa magharibi tu usiopatwa na jua mwanzo wa mchana, isipokuwa uko katikati kwenye sehemu ya ardhi, haukuelekea Mashariki wala Magharibi. Yanakaribia mafuta yake kwa usafi wake kuwaka yenyewe bila ya kuguswa na moto, na pindi yakiguswa na moto hung’ara mn’garo mkali mno, nuru juu ya nuru. Hiyo ni nuru kutokana na mwangaza utokao kwenye mafuta, ulioko juu ya nuru itokanayo na kuwasha moto. Basi huo ndio mfano wa uongofu, huwa unang’ara ndani ya moyo wa mwenye Imani. Na Mwenyezi Mungu Anamuongoza na kumuelekeza kuifuata Qur’ani Amtakaye, na Anawapigia watu mifano ili wapate kuifahamu mifano yake na hekima zake. Na Mwenyezi Mungu kwa kila kitu ni Mjuzi mno na hakuna chochote kinachofichamana Kwake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek