Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 36 - النور - Page - Juz 18
﴿فِي بُيُوتٍ أَذِنَ ٱللَّهُ أَن تُرۡفَعَ وَيُذۡكَرَ فِيهَا ٱسۡمُهُۥ يُسَبِّحُ لَهُۥ فِيهَا بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأٓصَالِ ﴾
[النور: 36]
﴿في بيوت أذن الله أن ترفع ويذكر فيها اسمه يسبح له فيها﴾ [النور: 36]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Nuru hii inayong’ara kwenye misikiti ambayo Mwenyezi Mungu Ameamrisha itukuzwe, ijengwe na jina Lake litajwe humo kwa kusoma Kitabu Chake na kuleta tasbihi (subhān Allāh) na kuleta tahlili (Allāh Akbar) na yasiyokuwa hayo katika aina mbalimbali za kumtaja. Wanaswali kwenye misikiti hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni |