Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 44 - النور - Page - Juz 18
﴿يُقَلِّبُ ٱللَّهُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ ﴾
[النور: 44]
﴿يقلب الله الليل والنهار إن في ذلك لعبرة لأولي الأبصار﴾ [النور: 44]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa ushahidi wa kutolea dalili uweza wa Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, kwamba Yeye Anaugeuza usiku na mchana kwa kuja mmoja wapo baada ya mwingine na kutafautiana kwao kwa urefu na ufupi. Katika hilo pana ushahidi kwa mtu mwenye busara na kuizingatia |