×

Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu huyasukuma mawingu, kisha huyaambatisha, kisha huyafanya 24:43 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nur ⮕ (24:43) ayat 43 in Swahili

24:43 Surah An-Nur ayat 43 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 43 - النور - Page - Juz 18

﴿أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُزۡجِي سَحَابٗا ثُمَّ يُؤَلِّفُ بَيۡنَهُۥ ثُمَّ يَجۡعَلُهُۥ رُكَامٗا فَتَرَى ٱلۡوَدۡقَ يَخۡرُجُ مِنۡ خِلَٰلِهِۦ وَيُنَزِّلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن جِبَالٖ فِيهَا مِنۢ بَرَدٖ فَيُصِيبُ بِهِۦ مَن يَشَآءُ وَيَصۡرِفُهُۥ عَن مَّن يَشَآءُۖ يَكَادُ سَنَا بَرۡقِهِۦ يَذۡهَبُ بِٱلۡأَبۡصَٰرِ ﴾
[النور: 43]

Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu huyasukuma mawingu, kisha huyaambatisha, kisha huyafanya mirundi? Basi utaona mvua ikitoka kati yake. Na huteremsha kutoka juu kwenye milima ya mawingu mvua ya mawe, akamsibu nayo amtakaye na akamuepusha nayo amtakaye. Hukurubia mmetuko wa umeme wake kupofua macho

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ألم تر أن الله يزجي سحابا ثم يؤلف بينه ثم يجعله ركاما, باللغة السواحيلية

﴿ألم تر أن الله يزجي سحابا ثم يؤلف بينه ثم يجعله ركاما﴾ [النور: 43]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kwani hukuona kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kutukuka, Anayapeleka mawingu pale Anapopataka, kisha Anayakusanya baada ya kuwa mbalimbali, kisha anayafanya yapandane na yarundikane, kisha Anaiteremshe mvua kutoka kwenye mrundiko huo? Na Anateremsha, kutoka kwenye mawingu yanayofanana na milima ya mawe kwa ukubwa wake, mvua ya barafu, Akaipeleka kwa amtakaye kati ya waja Wake na Akaiyondosha kwa Amtakaye kati yao kuambatana na hekima Yake na mpango Wake. Unakaribia mwangaza wa umeme huo umemetekao huko mawinguni, kwa ukali wake, kuyapofua macho ya wenye kuutazama
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek