Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 52 - النور - Page - Juz 18
﴿وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَخۡشَ ٱللَّهَ وَيَتَّقۡهِ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَآئِزُونَ ﴾
[النور: 52]
﴿ومن يطع الله ورسوله ويخش الله ويتقه فأولئك هم الفائزون﴾ [النور: 52]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika kufuata maamrisho na kujiepusha na makatazo na akaogopa mwisho mbaya wa uasi na akajihadhari na adhabu ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio wenye kufuzu kupata neema Peponi |