Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 60 - النور - Page - Juz 18
﴿وَٱلۡقَوَٰعِدُ مِنَ ٱلنِّسَآءِ ٱلَّٰتِي لَا يَرۡجُونَ نِكَاحٗا فَلَيۡسَ عَلَيۡهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعۡنَ ثِيَابَهُنَّ غَيۡرَ مُتَبَرِّجَٰتِۭ بِزِينَةٖۖ وَأَن يَسۡتَعۡفِفۡنَ خَيۡرٞ لَّهُنَّۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ ﴾
[النور: 60]
﴿والقواعد من النساء اللاتي لا يرجون نكاحا فليس عليهن جناح أن يضعن﴾ [النور: 60]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanawake wakongwe ambao wamejikalia hawajistareheshi na hawana matamanio kwa sababu ya uzee wao, hawana hamu ya kuolewa na wanaume wala wanaume hawana hamu nao. Wanawake hawa hawana makosa kujitanda sehemu ya nguo zao kama vile shuka, bila kuonesha pambo wala kujirembesha. Na kuvaa kwao nguo hizi, kwa kujisitiri na kujihifadhi, ni uzuri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi wa maneno yenu, ni Mjuzi wa nia zenu na matendo yenu |