×

Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya 24:61 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nur ⮕ (24:61) ayat 61 in Swahili

24:61 Surah An-Nur ayat 61 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 61 - النور - Page - Juz 18

﴿لَّيۡسَ عَلَى ٱلۡأَعۡمَىٰ حَرَجٞ وَلَا عَلَى ٱلۡأَعۡرَجِ حَرَجٞ وَلَا عَلَى ٱلۡمَرِيضِ حَرَجٞ وَلَا عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمۡ أَن تَأۡكُلُواْ مِنۢ بُيُوتِكُمۡ أَوۡ بُيُوتِ ءَابَآئِكُمۡ أَوۡ بُيُوتِ أُمَّهَٰتِكُمۡ أَوۡ بُيُوتِ إِخۡوَٰنِكُمۡ أَوۡ بُيُوتِ أَخَوَٰتِكُمۡ أَوۡ بُيُوتِ أَعۡمَٰمِكُمۡ أَوۡ بُيُوتِ عَمَّٰتِكُمۡ أَوۡ بُيُوتِ أَخۡوَٰلِكُمۡ أَوۡ بُيُوتِ خَٰلَٰتِكُمۡ أَوۡ مَا مَلَكۡتُم مَّفَاتِحَهُۥٓ أَوۡ صَدِيقِكُمۡۚ لَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَأۡكُلُواْ جَمِيعًا أَوۡ أَشۡتَاتٗاۚ فَإِذَا دَخَلۡتُم بُيُوتٗا فَسَلِّمُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمۡ تَحِيَّةٗ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِ مُبَٰرَكَةٗ طَيِّبَةٗۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ ﴾
[النور: 61]

Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu nyinyi, mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za kaka zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za shangazi zenu, au nyumba za wajomba zenu, au nyumba za dada wa mama zenu, au za mlio washikia funguo zao, au rafiki yenu. Si vibaya kwenu mkila pamoja au mbali mbali. Na mkiingia katika nyumba, toleaneni salamu, kuwa ni maamkio yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu, yenye baraka na mema. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kubainishieni Aya zake mpate kuelewa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ليس على الأعمى حرج ولا على الأعرج حرج ولا على المريض حرج, باللغة السواحيلية

﴿ليس على الأعمى حرج ولا على الأعرج حرج ولا على المريض حرج﴾ [النور: 61]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hawana dhambi watu wenye nyudhuru miongoni mwa vipofu, viguru na wagonjwa, kuyaacha mambo ya lazima ambayo hawawezi kuyatekeleza, kama kupigana jihadi na mfano Wake katika vitu ambavyo vinahitajia kwa kipofu awe huona na kiguru awe mzima na mgonjwa awe na afya nzuri. Na nyinyi, enyi Waumini, hamuna makosa kula kwenye majumba ambayo ndani yake kuna wake zenu na watoto wenu, na hapa yanaingia majumba ya watoto, au majumba ya baba zenu au mama zenu au ndugu zenu wa kiume au dada zenu au ami zenu au mashangazi zenu au wajomba zenu au mama zenu wadogo au kwenye nyumba ambazo mliwakilishwa kuzisimamia wakati wenyewe hawapo kwa ruhusa yao au kwenye nyumba za marafiki. Hakuna makosa yoyote kwenu kula mkiwa pamoja au mbalimbali. Na muingiapo kwenye nyumba zinazokaliwa au zisizokaliwa, amkianeni nyinyi kwa nyinyi kwa maamkizi ya Kiislamu, nayo ni «As-salāmu ‘alaikum wa rahmatullāhi wa barakātuh, au As-salāmu ‘alainā wa ‘alā ‘ibādillāhi-s-sālihīn, iwapo hakuna yoyote. Maamkizi haya Mwenyezi Mungu Ameyaweka, nayo yana baraka, yanakuza kusafiana nia na kupendana, ni mazuri yanayopendeza kwa mwenye kuyasikia. Na kwa mfano wa ufafanuzi huu anawafafanulia Mwenyezi Mungu alama za Dini Yake na aya Zake, ili mzifahamu na mzitumie
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek