Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 59 - النور - Page - Juz 18
﴿وَإِذَا بَلَغَ ٱلۡأَطۡفَٰلُ مِنكُمُ ٱلۡحُلُمَ فَلۡيَسۡتَـٔۡذِنُواْ كَمَا ٱسۡتَـٔۡذَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ﴾
[النور: 59]
﴿وإذا بلغ الأطفال منكم الحلم فليستأذنوا كما استأذن الذين من قبلهم كذلك﴾ [النور: 59]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na pindi watoto wanapofikia miaka ya kubaleghe na kukalifishwa hukumu za kisheria, ni juu yao watake ruhusa wakitaka kuingia nyakati zote kama wanavyotaka ruhusa watu wazima. Na kama Mwenyezi Mungu Anavyowafafanulia adabu za kutaka ruhusa (kuingia majumbani), vilevile Anawafafanulia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, aya Zake. Na Mwenyezi Mungu Anayajua sana yanayowafaa waja Wake, ni Mwingi wa hekima katika sheria Zake |