Quran with Swahili translation - Surah An-Nur ayat 64 - النور - Page - Juz 18
﴿أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ قَدۡ يَعۡلَمُ مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ وَيَوۡمَ يُرۡجَعُونَ إِلَيۡهِ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُواْۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ ﴾
[النور: 64]
﴿ألا إن لله ما في السموات والأرض قد يعلم ما أنتم عليه﴾ [النور: 64]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Jueni mtanbahi kwamba ni vya Mwenyezi Mungu vilivyoko mbinguni na ardhini, kwa kuviumba, kuvimiliki, kuvifanya vimdhalilikie. Ujuzi Wake umevizunguka vyote ambavyo muko navyo. Na Siku ya Akhera, ambayo waja watarejea Kwake, Atawapa habari ya matendo yao, na Atawalipa kwayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu, hayafichamani Kwake Yeye matendo yao na hali zao |