Quran with Swahili translation - Surah Al-Furqan ayat 18 - الفُرقَان - Page - Juz 18
﴿قَالُواْ سُبۡحَٰنَكَ مَا كَانَ يَنۢبَغِي لَنَآ أَن نَّتَّخِذَ مِن دُونِكَ مِنۡ أَوۡلِيَآءَ وَلَٰكِن مَّتَّعۡتَهُمۡ وَءَابَآءَهُمۡ حَتَّىٰ نَسُواْ ٱلذِّكۡرَ وَكَانُواْ قَوۡمَۢا بُورٗا ﴾
[الفُرقَان: 18]
﴿قالوا سبحانك ما كان ينبغي لنا أن نتخذ من دونك من أولياء﴾ [الفُرقَان: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hapo waabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu watasema, «Kutakasika ni kwako, ewe Mola wetu! Tunajiepusha na kitendo walichokifanya hawa. Haipasii kwetu sisi kuwategemea wasaidizi wa kutusaidia isipokuwa wewe. Lakini wewe uliwasterehesha hawa washirikina na baba zao kwa mali na afya nzuri, mpaka wakasahau utajo wako wakakushirikisha, na wakawa ni watu walioangamia walioghilibiwa na ubaya na hizaya.» |