Quran with Swahili translation - Surah An-Naml ayat 19 - النَّمل - Page - Juz 19
﴿فَتَبَسَّمَ ضَاحِكٗا مِّن قَوۡلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوۡزِعۡنِيٓ أَنۡ أَشۡكُرَ نِعۡمَتَكَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَٰلِدَيَّ وَأَنۡ أَعۡمَلَ صَٰلِحٗا تَرۡضَىٰهُ وَأَدۡخِلۡنِي بِرَحۡمَتِكَ فِي عِبَادِكَ ٱلصَّٰلِحِينَ ﴾
[النَّمل: 19]
﴿فتبسم ضاحكا من قولها وقال رب أوزعني أن أشكر نعمتك التي أنعمت﴾ [النَّمل: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Akatabasamu akicheka kwa neno la huyu chungu, kwa kufahamu kwake na kuwa na akili ya kuwaonya chungu, na akatambua neema ya Mwenyezi Mungu juu yake. Hapo akaelekea Kwake akiomba, «Mola wangu! Nipe muelekeo na uniafikie nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu wawili, na nifanye matendo mema ambayo wewe utaridhika nayo kutoka kwangu na unitie, kwa rehema zako, ndani ya starehe ya Pepo yako pamoja na waja wako wema ambao uliridhika na matendo yao |