Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 50 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿فَإِن لَّمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَكَ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَمَنۡ أَضَلُّ مِمَّنِ ٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ بِغَيۡرِ هُدٗى مِّنَ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[القَصَص: 50]
﴿فإن لم يستجيبوا لك فاعلم أنما يتبعون أهواءهم ومن أضل ممن اتبع﴾ [القَصَص: 50]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wasipokuitikia kwa kuleta Kitabu, na hawakusaliwa na hoja yoyote, basi ujue kwamba wao wanafuata matamanio yao. Na hakuna yoyote aliye mpotevu zaidi kuliko yule aliyefuata matamanio yake bila ya kuwa na uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Hawaafikii kuifikilia haki watu madhalimu walioenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na wakakiuka mipaka Yake |