Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 13 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿وَلَيَحۡمِلُنَّ أَثۡقَالَهُمۡ وَأَثۡقَالٗا مَّعَ أَثۡقَالِهِمۡۖ وَلَيُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ عَمَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 13]
﴿وليحملن أثقالهم وأثقالا مع أثقالهم وليسألن يوم القيامة عما كانوا يفترون﴾ [العَنكبُوت: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wataibeba, tena wataibeba, washirikina hawa mizigo ya nafsi zao na madhambi yake na mizigo ya wale waliowapoteza na wakawazuia wasiifuate njia ya Mwenyezi Mungu pamoja na mizigo yao wenyewe, bila ya wale waliowafuata nyinyi kupunguziwa mizigo yao kitu chochote. Na wataulizwa, tena wataulizwa, Siku ya Kiyama, kuhusu yale ya urongo waliokuwa wakiyazua |