Quran with Swahili translation - Surah Al-‘Ankabut ayat 12 - العَنكبُوت - Page - Juz 20
﴿وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّبِعُواْ سَبِيلَنَا وَلۡنَحۡمِلۡ خَطَٰيَٰكُمۡ وَمَا هُم بِحَٰمِلِينَ مِنۡ خَطَٰيَٰهُم مِّن شَيۡءٍۖ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ ﴾
[العَنكبُوت: 12]
﴿وقال الذين كفروا للذين آمنوا اتبعوا سبيلنا ولنحمل خطاياكم وما هم بحاملين﴾ [العَنكبُوت: 12]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanasema wale waliokataa upweke wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Makureshi, na wasiliamini onyo la Mwenyezi Mungu na ahadi Yake, kuwaambia wale waliomuamini Mwenyezi Mungu miongoni mwao na wakafuata Sharia Zake kivitendo, «Iacheni Dini ya Muhammad, na fuateni dini yetu, kwani sisi tutayabeba makosa yenu,» na wao si wenye kubeba chochote katika dhambi zao. Kwa kweli, wao ni warongo kwa yale waliyoyanena |