Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 117 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿مَثَلُ مَا يُنفِقُونَ فِي هَٰذِهِ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا كَمَثَلِ رِيحٖ فِيهَا صِرٌّ أَصَابَتۡ حَرۡثَ قَوۡمٖ ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فَأَهۡلَكَتۡهُۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ ٱللَّهُ وَلَٰكِنۡ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ ﴾
[آل عِمران: 117]
﴿مثل ما ينفقون في هذه الحياة الدنيا كمثل ريح فيها صر أصابت﴾ [آل عِمران: 117]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mfano wa wanachokitoa makafiri, katika mambo ya kheri, katiika maisha haya ya ulimenguni na thawabu wanazozitumaini, ni mfano wa upepo ulio na baridi kali uliovuma juu ya mashamba ya watu waliokuwa wanangojea kwa hamu matokeo mema ya upepo huo. Na kwa sababu ya madhambi yao, upepo huo haukubakisha chochote. Na makafiri hawa, hawatapata thawabu huko Akhera. Na Mwenyezi Mungu hatakuwa Amewadhulumu kwa hilo, lakini ni wao walijidhulumu nafsi zao kwa ukafiri wao na kuasi kwao |